Tuendelee,kama utakumbuka vizuri ni siku chache tu toka Tume ya vyuo vikuu nchini ikishirikiana na NACTE kutangaza rasmi utaratibu wa namna ya kutuma maombi vyuo mbalimbali ikiwa ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwombaji alipaswa kuomba kupitia Central admission system ya TCU NA NACTE,
Kutokana na changamoto zilizowahi kujitokeza hapo mwanzo, kwa mwaka huu wa masomo 2017/2018 waombaji watatuma maombi chuoni moja kwa moja kulingana na maelekezo ya chuo.
Lakini tukiachilia mbali suala hilo, wengi nadhani mnasubiri kwa shauku kuu ya kufunguliwa kwa dirisha kwa waombaji wapya ili waanze kutuma maombi na ambapo pia tu juzi bodi ya mikopo ilidokeza kidogo mabadiliko ambayo inatarajia kuyafanya ikiwa ni maboresho ya mfumo wa zamani..
Kila anayeomba mkopo bodi ya mikopo (HESLB) matajario yao ni kupata huo mkopo lakini usije shangaa pamoja na kuwa na sifa zote za kuupata mkopo utajikuta umekosa, unafikiri kwa nini?.
Ungana nami hapa nikupe A-Z ya kwanini utakosa mkopo na kwa nini utapata mkopo wa serikali kwa ajili ya masomo yako..
Mambo yafuatayo ukiyafanya sahau kupata huo mkopo hata kama utakua na division one ya 3.
1.Kuchagua kozi ambazo siyo vipaumbele vya taifa.
Kozi fulani kupewa kipaumbele katika kupewa mikopo haina maana ya kwamba kozi zingine hazina umuhimu sana bali ni mpango wa taafa kuaandaa wataalamu wanaohitajika kwa muda husika katika sekta husika. Hivyo wewe kama mwombaji jitahidi kufanya tafiti kujua ni kozi zipi hupewa vipaumbele katika utoajia wa mikopo. Kwa mfano Mwaka jana 2016/2017 education programmes nyingi za sayansi na hisabati wanafunzi waliomba kozi hizo walikua na uwezekano mkubwa wa kupata mkopo ukiachilia mbali bajeti ya serikali kwa mwaka huo.
2.Taarifa sahihi wakati wakutuma maombi.
Hapa pia kuna changamoto zake. Watu wengi hujidanganya eti ukiwa yatima lazima upate mkopo japokua ni kweli hua hivyo lakini cha ajabu ambacho hutokea ni kwamba watu hufany forgery ya vyeti vya vifo na vya kuzaliwa ili wapewe mikopo. Ikumbukwe kwamba forgery yoyote ni kosa kisheri ikigundulika. Toa taarifa sahihi kuepusha usumbufu utakaojitokeza mbele ikumbukwe kuna maisha baada ya kupewa mkopo.
3.Ujazaji wa fomu ya kuomba mikopo ikiwa haijakamilika ( incomplete)
Imekua ikijirudia mara kwa mara bodi kutoa orodha ya majina ya waombaji ambao fomu zao zilituma zikiwa hazijajazwa taarifa zote. Kwa mfano form kuwasilishwa bodi bila muhuri wa mwenyekiti wa kitongoji, muhuri wa mahakama,bila sahihi ya mwombaji n.k mambo haya yote yanapunguza uwezekano wa kupata mkopo licha ya kwamba utakua na matokeo mazuri.
3.Kutokusoma vigezo na masharti ya ya Bodi.
Ni jambo ambalo ni common kwa sisi wote kutokusoma vizur na kwa umakini masharti ya bodi mbaya zaidi tunspenda kusimuliwa na wenzetu. Ukituma maombi bila ya kuwa na ufahamu wa kutosha wa maelekezo na masharti yatakayotolewa na bodi ..Uwezekano wa wewe kupata huo mkopo utapungua sana. Jitahidi kusoma vizuri maelekezo kabla ya kuanza kutuma maombi ya huo mkopo.
4.Viambatanisho muhimu.
Fomu ya maombi ya mkopo itakutaka uambatanishe vivuli vya vyeti mbalimbali au kitambulisho.Hakikisha unaambatanisha kadri ya maelekezo uliyopewa na Bodi.
Mwisho kabisa nikutakie maandalizi mema ya kuingia katika ulimwengu wa wasomi duniani.Ukipata nafasi ya kupata mkopo basi utumie vizuri ukikumbuka kwamba mara baada ya kuhitimu masomo yako ya chuo kikuu utahitajika kuurejesha kwa makato ya asilimia 15 ya mshahara wako Usikwende kula bata sana Mkuu.
Best wishes.
Alhamisi, 3 Agosti 2017
Mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya loan board application
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni